Mon - Fri: 8:00 - 15:00
Working Hours
+255 784 577 115
Hotline
P.O.Box 907 , Tanga, Tanzania
Maranzara, Pongwe

1. SHULE YA WASICHANA YA KIISLAMU YA PONGWE

Ni shule ya bweni kwa wasichana tu, kuanzia Kidato I - IV. Shule ipo Tanga mjini- umbali wa kilometa mbili (2) toka Pongwe karibu na shule ya Msingi Maranzara.Unaweza kufika shuleni kwa usafiri wa pikipiki kwa gharama ya shilingi (1000/=) kutokea Kituo cha basi Pongwe, Barabara kuu ya Tanga-Segera.

Mbali na kutoa elimu ya sekondari, shule imedhamiria;
  1. Kuwawezesha mabinti wa Kiislamu kuitambua hadhi na Jukumu lao katika jamii.
  2. Kuwaelimisha na kuwalea mabinti, ili kupata viongozi bora wa baadae katika ngazi ya familia na Taifa kwa ujumla.
  3. Kujenga msingi wa wataalamu wa kike katika fani za sayansi ikiwemo utabibu.

2. MASOMO YANAYOFUNDISHWA

Shule inafundisha kwa Mtaala wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Tanzania. Masomo yanayofundishwa ni, Maarifa ya Uislamu, Mathematics, English Language, Arabic Language, Literature in English, Physics, Chemistry, Biology, Geography, History na Civics.

Shule inafundisha elimu ya Dini ya Kiislamu kwa mfumo wa Madrassa ikiwemo Qur’an (Hifdh na Tilawat), Hadith, Tawheed, Fiqh na Sirat kwa Lugha ya Kiarabu.

3. SARE YA SHULE

Wanafunzi watakaodahiliwa shuleni hapa hawataruhusiwa kuja na nguo zaidi ya zitakazo ainishwa katika jedwali lifuatalo;
SARE ZINAZOHITAJIKA
RANGI YA VAZI
(A)  SARE YA DARASANI
Suruali (Panjabi) mbili (2)
Darkish Blue
Ushungi mkubwa wa mviringo wa chini ya goti.
Nyeupe
Nusu kanzu mbili (2) chini ya goti na mikono mirefu
Darkish Blue
Baibui moja (1) itakayovaliwa juu baada ya suruali na nusu kanzu
Darkish Blue
Viatu vya kufunika mguu visivyo na kisigino kirefu vyenye kamba (Kisigino wastani wa nchi 1)
Vyeusi
Soksi jozi mbili (2)
Nyeupe
(B)  SARE YA NJE YA DARASA
Baibui lisilopasuliwa mbele. Mpira mzito
Blue Masai
Ushungi mkubwa wa mviringo wa chini ya goti.
Blue Masai
Suruali ya kuvalia shamba.
Jozi (1) Kanga na Kitenge, Baibui jeusi na shungi lake. (Aje nalo kuvaa akisubiri sare)
Nyeusi
Simple Raba (Aje nazo) haturuhusu open shoes zaidi ya ndala za kuogea
Maruni

4. VIFAA VYA MASOMO NA BWENINI VINATOLEWA SHULENI

Kila mwanafunzi analazimika kuwa na vifaa vya masomo ambavyo vitatolewa na shule gharama (199,000/=) imeainishwa hapo chini;

  1. Godoro 45,000/=
  2. Shuka 2 = 16,000/=
  3. Trunk 25,000/=
  4. Daftari 15 (3 Quires 10 @ 3,000 na 4 Quire 5 @ 3,500)
  5. Chandarua 12,000/=
  6. Rimu A4 16,000/= na Rimu ya mistari 9,000/=
  7. Mkebe 2,500
  8. Jembe na mpini 8,000
  9. Ndoo, beseni,sahani, kikombe na bakuli 10,000
  10. Graph paper 2 @ 2,500
  11. Seti ya penseli za rangi 3,000

5. VIFAA VYA HOSTELI

  1. Taulo, malapa na mswaki.
  2. Chupa ya kuhifadhia maji ya moto
  3. Sabuni ya kufulia na kuogea.
  4. Sweta la kufuma rangi blue (kuvaa wakati wa baridi)
  5. Mini Whiteboard 1, Past it Note dozen 1
  6. Msahafu
  7. Mkoba wa Madaftari (Begi Jeusi)
  8. Kalamu za kutosha
NB. Mwanafunzi atakapoacha, kufukuzwa au kuhama shule vifaa vyake kama vile godoro sanduku n.k anatakiwa kuondoka navyo.

6. ADA NA MICHANGO YA SHULE

Mwanafunzi anatakiwa kulipa ada ya shule ya mwaka wa masomo 2023 kwa utaratibu ufuatao,
  • Alipe ada yote kwa mwaka Tsh 1,850,000/=
  • Alipe kwa awamu tatu kama inavyoainishwa katika jedwali hapo chini. Malipo Yanafanywa Wiki ya Kwanza ya Mwezi Tajwa
                 1. Awamu ya kwanza:  Januray (Tsh. 800,000/=)   
                 2. Awamu ya pili:  Januray (Tsh. 650,000/=) 
                 3. Awamu ya tatu:  Januray (Tsh. 400,000/=) 
  • Mwanafunzi ambaye hana bima ya afya aje na shilingi elfu sitini (60,000/=) kwa ajili ya kulipia bima hiyo.
  • Wanafunzi wa kidato cha kwanza 2023 wanalazimika kulipa 250,000/= kwa ajili ya iPad (Kishikwambi) kwa kuwa ufundishaji na ujifunzaji utatumia teknolojia.
  • Malipo ya ada yafanyike kupitia AMANA BANK Akaunti Namba 008121053180001 au DIAMOND TRUST BANK (DTB) Akaunti Namba 0035678001, Jina la Akaunti PONGWE ISLAMIC GIRLS SECONDARY SCHOOL.
AINA YA MCHANGO
KIASI (TZS)
Usajili
10,000.00
Ukarabati
10,000.00
Nembo ya shule (1)
5,000.00
Kitambulisho
5,000.00
Mahafali Kidato IV- 2020
15,000.00
Ukaguzi na Michezo
10,000.00
Mitihani ya Kila wiki
10,000.00
Sare za Shule jozi 2 @ 75,000/=
150,000.00
Sare ya Kushindia jozi 2 @ 40,000/=
80,000.00
JUMLA KUU
295,000.00

7. UANDIKISHWAJI

Siku ya kuripoti shuleni mwanafunzi awe na vifaa vifuatavyo:

  1. Fomu za maelezo ya mzazi / mlezi kuhusu utambulisho wa mwanafunzi na wazazi / walezi (Kiambatanisho A)
  2. Maelezo yaliyothibitishwa na Daktari (Medical Examination Report) kama mwanafunzi ana matatizo ya kiafya au la (Kiambatanisho B).
  3. Stakabadhi ya Malipo ya Benki (Pay in Slip)
  4. Rimu mbili (2), (A4) moja na Karatasi zenye mistari (Ruled Paper) moja.
  5. Picha tatu (3) za passport size au TShs 2000/=.
  6. Uthibitisho wa Kumaliza Darasa la Saba (VII) (Namba ya PLSE)
  7. Fagio la njiti, jembe na mpini kwa ajili ya usafi wa mazingira.
  8. Nakala ya Cheti cha Kuzaliwa.

8. MAENDELEO YA DARASANI

Ili kufaulu kuingia Kidato II mwanafunzi anatakiwa afikishe wastani wa alama zisizopungua 55% na Credit saba (7) au zaidi kwa mwanafunzi atakaeingia Kidato IV. Somo la Maarifa ya Uislamu na Lugha ya Kiarabu yanachukua uzito wa pekee hivyo kila mwanafunzi analazimika kufanya bidii na kuhakikisha anafaulu angalau kwa kiwango cha daraja ‘B’.

9. KUTEUA MASOMO

  1. Mwanafunzi atakayefaulu kuingia Kidato cha Tatu atachagua masomo katika mchepuo wa Sayansi na Sanaa (Arts) tu.
  2. Uchaguzi wa masomo utazingatia uwezo wa mwanafunzi, utashi wake, ushauri wa Wazazi/Walezi na waalimu wa masomo husika atakuwa na nafasi kubwa zaidi katika maamuzi hayo.

10. KUTEMBELEA WANAFUNZI

Shule inatoa fursa kwa wazazi /walezi kutembelea wanafunzi kila Jumapili ya mwisho wa mwezi isipokuwa kipindi cha mitihani. Pamoja na ruhusa hiyo mzazi/ mlezi haruhusiwi kumletea mwanafunzi chakula cha aina yoyote.

11. KANUNI NA MWENENDO BORA WA SHULE

  1. Wanafunzi wote wanapaswa kufahamu kuwa chochote kilicho nje ya maadili mema hakina nafasi hapa shuleni.
  2. Kila mwanafunzi hana budi kujipamba na vipengele vya tabia njema.
  3. Kila mwanafunzi atawajibika kuzingatia na kufuata kikamilifu ratiba na kalenda ya shule.
  4. Mwanafunzi atakuwa kajifukuzisha shule mwenyewe iwapo hatafika shule kwa siku ishirini na moja (21) bila taarifa zozote shuleni. Taarifa iwe kabla na wala si baada ya tukio la utoro.
  5. Wakati wa masomo wanafunzi wote watabaki shuleni, hawataruhusiwa kutoka ndani ya shule isipokuwa kwa kibali maalum.
  6. Mwanafunzi atakaekuwa na Wastani wa mahudhurio chini ya asilimia themanini na moja (81%) hatoruhusiwa kufanya mtihani, hivyo hatoruhusiwa pia kuendelea na Kidato kinachofuata, baadala yake atarudia mwaka au kufukuzwa shule.
  7. Wakati wote wa kuwa shule, vazi rasmi ni sare ya shule, kinyume chake ni kosa. Mwanafunzi atavaa na kuzingatia maadili hata awapo nje ya shule.
  8. Mwanafunzi ataripoti tatizo kwanza kwa Head Girl kisha ndipo amwone Mwalimu wa zamu, darasa au nidhamu.
  9. Kelele au zogo hairuhusiwi katika eneo la shule, mazungumzo yote hayanabudi kufuata nidhamu na maadili.
  10. Hairuhusiwi wanafunzi kuja shuleni na chakula cha aina yoyote ama kuletewa zawadi ya chakula na mzazi/mlezi wakati atakapotembelewa.
  11. Ni marufuku kwa mwanafunzi kujipamba kwa rangi za kucha, nywele, midomo, kupaka wanja, kunyoa nyusi, kuvaa hereni, bangili, mkufu au pete.
  12. Hairuhusiwi kufanya sherehe za Birtdhday na au Valentine Day kwa namna yoyote shuleni.
  13. Hairihusiwi kulala zaidi ya mwanafunzi mmoja katika kitanda kimoja.
  14. Vifaa vya electronics kama vile simu au line, mp3, ipod, camera, radio, radio cassette n.k haviruhusiwi mwanafunzi kuwa navyo katika mazingira ya shule.
  15. Mbali na kuvunja kanuni hizi halali za shule mwanafunzi atajifukuzisha shule mwenyewe iwapo atajihusisha na ulevi, uesherati na uzinifu.

❖ Mamlaka ya shule ndio yenye maamuzi ya mwisho katika kutekeleza kanuni hizi.

12. MAKOSA YANAYOWEZA KUSABABISHA KUFUKUZWA SHULE

Pamoja na maelezo yote hayo. Mwanafunzi atakayechupa kwa makusudi maadili na kanuni za shule kwa kutenda makosa makubwa kama yalivyoainishwa hapo chini atafukuzwa shule:
  1. Kunywa pombe
  2. Kwenda nyumba za starehe kama vile kwenye kumbi za madansi, disko n.k
  3. Uzinzi,ushoga au kukaribia zinaa kwa namna yeyote.
  4. Kuvuta bangi, madawa ya kulevya, n.k
  5. Kutosimamisha swala.
  6. Kumiliki vitu vya electronics kama simu au line, mp3, ipod, radio, kamera n.k
  7. Kutoroka shuleni
  8. Kugoma adhabu stahiki kwa makusudi.
  9. Kupata mimba au kutoa mimba ndani na nje ya shule
  10. Kuanzisha, kuchochea, kushiriki au kuongoza mgomo.
  11. Kuhatarisha amani ya shule kwa kupigana au kuchochea watu wapigane
  12. Wizi, uporaji na uharibifu wa mali ya shule na ya wanafunzi au wakazi wa kituo.
  13. Kukosa mitihani/jaribio bila ya sababu za msingi.
  14. Kutohudhuria masomo/darasani bila sababu maalumu za msingi.

13. HITIMISHO

Ni matumaini yetu kuwa Mzazi/ Mlezi na mwanafunzi mtarajiwa mmeyasoma maelezo haya kwa makini tayari kwa utekelezaji.

Baada ya kujiunga na shule utekelezaji wa kanuni na taratibu za shule kwa mwanafunzi na Mzazi/Mlezi ni wajibu.

Mzazi / Mlezi mlete mwanao PONGWE ISLAMIC GIRLS SECONDARY SCHOOL yenye mazingira mazuri ya kimalezi ili aweze kupata masomo na maadili mema kwa maslahi ya mtoto, wazazi, na jamii kwa ujumla.

TUNAKUTAKIA MAISHA MEMA NA KARIBU SANA
Visitors' Statistics

Today 8 - Yesterday 34

Enquiry Form